loader
Mambo ya Ndani washauriwa kufanyakazi kwa weledi

Mambo ya Ndani washauriwa kufanyakazi kwa weledi

Waziri Chikawe aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha majadiliano ya bajeti ya mwaka 2013/2014 na mambo yanayotarajiwa kufanywa na wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2014/2015.

“Nitoe mwito kwenu, watumishi wote kushirikiana na kujituma kufanya kazi kwa bidii, kila mtu kwa nafasi yake aliyonayo ili hatimae wizara yetu hii iweze kufikia malengo tuliyojiwekea kwa mwaka ujao wa fedha,” alisema Waziri Chikawe.

Aliwataka wafanyakazi hao kuhakikisha wanatumia kikao hicho kujadili masuala ya msingi ambayo waliyafanya mwaka wa fedha uliopita na pia kupanga mambo mengine ya mwaka wa fedha 2014/2015 ili kufikia malengo yao.

Aidha, Waziri Chikawe alikabidhi zawadi kwa mfanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye ametoka Jeshi la Polisi, Isack Lukita ambaye amewezesha polisi kuokoa fedha nyingi za wizara.

Lukita alikabidhiwa Sh milioni mbili kwa kuwa mfanyakazi bora ambaye ameisaidia wizara kuokoa fedha, ikiwa ni pamoja na kutengeneza kemikali ya kutambua namba za magari yaliyoibiwa.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments