loader
Dstv Habarileo  Mobile
Manyoni wakamata nyara za mil 202.5/-

Manyoni wakamata nyara za mil 202.5/-

Mkuu wa wilaya ya Manyoni, Fatma Toufiq alitaja nyara hizo kuwa ni pamoja na vipande 28 vya meno ya tembo, ngozi moja ya simba, mabunda sita ya singa za tembo, mkia mmoja wa pofu na kucha nne za simba.

Pia zimekamatwa bunduki mbili za kijeshi aina ya SMG, risasi 48 za SMG na ‘magazine’ tatu zilikamatwa.

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mapambano dhidi ya ujangili wilayani humo.

Alisema kuwa uongozi wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na Kikosi cha Kuzuia Ujangili (KDU) ulifanikiwa kuwanasa watuhumiwa sita waliokutwa wakiwa na nyara pamoja na silaha hizo.

Toufiq alisema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 8, mwaka huu majira ya asubuhi kwenye nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la Manyoni mjini na kuongeza kuwa ukamataji wa watuhumiwa hao ulifanikiwa kutokana na taarifa za raia wema.

Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watuhumiwa kwa kile alichodai kuwa hatua hiyo ingeathiri uchunguzi unaoendelea. Mkuu huyo wa wilaya aliwashukuru wananchi wote wa wilaya hiyo kwa ushirikiano wao wa hali ya juu ambao alidai kuwa umerahisisha mapambano dhidi ya majangili katika wilaya ya Manyoni.

Wilaya ya Manyoni ina mapori ya akiba mbalimbali ikiwemo Rungwa, Kizingo na Muhesi.

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Manyoni

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi