loader
Marais EAC wakutana kujadili itifaki Soko la Pamoja

Marais EAC wakutana kujadili itifaki Soko la Pamoja

Katika mkutano huo wa siku moja, miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kutathmini hatua iliyofikiwa kuhusu utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja lililoanza rasmi Novemba 2009.

Itifaki ya Soko la Pamoja inaruhusu uhuru wa bidhaa, watu, ajira, huduma pamoja na mitaji kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ama kuishi au kufanya shughuli pasipo vikwazo.

Soko la Pamoja ni hatua ya pili katika ushirikiano wa kiuchumi ndani ya EAC, ikiwa imetanguliwa na Umoja wa Forodha uliotiwa saini 2005.

Hatua ya tatu ni Umoja wa Fedha uliotiwa saini Kampala, Uganda, Novemba, mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Sekretarieti ya EAC, marais hao watapokea marekebisho ya muundo wa kufikia hatua ya Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki, hatua ambayo ni ya mwisho katika lengo kuu la mtangamano wa EAC.

Mkutano huo pia utapitia maombi ya nchi za Sudan Kusini na Somalia kujiunga na EAC.

foto
Mwandishi: Mtuwa Salira, EANA

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi