loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mashamba Monduli kurudishwa kwa wananchi

Mashamba Monduli kurudishwa kwa wananchi

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa katika Kijiji cha Lemooti.

Alisema hayo muda mfupi baada ya kuzindua nyumba ya ghorofa moja na bwawa la maji, vyenye thamani ya Sh milioni 600, mali ya mfanyabiashara wa mifugo na mnunuzi wa madini ya tanzanite, Isaya Lembekule `Masikio’ katika kijiji hicho kilichopo Kata ya Lolkisale.

Alisema uhaba wa ardhi wilayani Monduli ni mkubwa, hivyo aliishauri Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kufanya utaratibu wa kufuta hati zote za mashamba hayo ili umiliki wa mashamba hayo, urejeshwe kwa uongozi wa vijiji.

Alisema hati zilizotolewa, zingine zilitolewa halali na nyingine upatikanaji wake unatia shaka, kwani baadhi ya mashamba hayo ambayo mengine yako karibu na makazi na hayaendelezwi, hivyo haina haja ya kuyaachia kuwa misitu, wakati wengine wana shida ya ardhi ya kilimo na kulisha mifugo.

‘’Naomba Halmashauri mfanye utaratibu wa kufuta hati zote za mashamba hayo haraka na umiliki wake urejeshwe kwa vijiji ili wananchi waweze kulima na hatimaye kulisha mifugo yao,’’ alisema.

Akizungumzia maendeleo kwa vijana wa jamii ya Kimasai, Lowassa alimsifu Lembekule kwa kujenga ghorofa la makazi yake katika Kijiji cha Lomooti, umbali wa zaidi ya kilomita 80 kutoka njia panda ya Monduli.

Aliwataka wengine kuiga mfano huo. Alisema amefurahishwa kuona ghorofa ya kisasa na nyumba nzuri ya mfanyabiashara huyo, mwenye ng’ombe wa kisasa 780 na ng’ombe wa kienyeji 960 katika kijiji hicho.

Alitoa mwito kwa wengine, kufanya kila linalowezekana kurudisha maendeleo vijijini na sio mijini tu.

WAZIRI wa Nishati, January Makamba ameseme wataalamu wa ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Monduli

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi