loader
Matumizi ya gesi yaipatia serikali bilioni 424.9/-

Matumizi ya gesi yaipatia serikali bilioni 424.9/-

Aidha shirika hilo, limebainisha kuwa kupitia gesi hiyo asilia katika eneo la uzalishaji umeme, hadi sasa kiasi cha megawati za umeme 562.5 kinazalishwa, lakini kinachotumika ni megawati za umeme 411, sawa na asilimia 40 ya umeme unaozalishwa katika gridi ya taifa. Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Masoko na Vitega Uchumi wa shirika hilo, Joyce Kisamo.

Alisema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya upatikanaji wa gesi asilia nchini katika semina ya waandishi wa habari, iliyofanyika mjini Bagamoyo mwishoni mwa wiki.

“Katika kipindi hiki, jumla ya Sh trilioni 9.4 ziliokolewa kutokana na matumizi hayo ya gesi asilia katika uzalishaji umeme dhidi ya umeme unaozalishwa na mafuta ambao una gharama kubwa,” alisema Kisamo.

Alisema hadi sasa Tanzania imebaini katika mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Pwani, kiasi cha futi za ujazo trilioni 50.5 za gesi ambazo kati yake futi za ujazo 42.5 zimegunduliwa katika maeneo ya kina kirefu cha bahari na futi za ujazo nane nchi kavu.

“Bado Serikali inaendelea na utaratibu wa kutafiti kupitia mikataba na kampuni mbalimbali zenye sifa katika maeneo yanayodhaniwa kuwa na rasilimali hiyo ya gesi asilia au mafuta,” alisisitiza.

Alisema kwa gesi iliyopatikana, Serikali imeweka mipango mingi, ambayo pamoja na kuisafirisha kwa matumizi ya nyumbani, nishati na viwandani na majumbani, pia wako katika mchakato wa kuanzisha maeneo ya viwanda vya gesi.

Alisema hadi sasa kupitia gesi inayozalishwa katika maeneo ya Songosongo na Mnazibay, jumla ya nyumba 30,000 ziko kwenye mchakato wa kufungiwa mfumo wa kutumia gesi, magari 8,000 ya majaribio yameanza kutumia gesi, na vituo 12 vya gesi tayari vimeshajengwa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo, James Andilile, alisema kadri gesi inavyoendelea kupatikana nchini, ndivyo kampuni za utafiti zinavyozidi kuongezeka, hali ambayo endapo gesi hiyo itaendelea kugundulika, itakuwa mkombozi wa uchumi kwa watanzania.

Alisema kuanzia mwaka 2004 hadi sasa, visima 78 vya gesi kupitia kampuni mbalimbali, vimechimbwa. Kati ya visima hivyo, katika eneo la kina kirefu, visima 24 vilibainika kuwa na gesi. Katika nchi kavu, visima vitatu vilibainika na nishati hiyo, sawa na asilimia 32.

“Kwa mwaka huu pekee, TPDC imepanga kuchimba visima 13 kwa ajili ya kutafiti mafuta au gesi,” alisisitiza.

Aliwatahadharisha Watanzania na waandishi wa habari, kuwa makini na taarifa zinazotolewa na watu wasio na nia nzuri na Tanzania, kuhusu masuala ya gesi, kwani rasilimali hiyo ikitumiwa vizuri, inaweza kuikomboa Tanzania, lakini, ikichezewa inaweza kuwa mwiba.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi