loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mbunge aahidi kutoa mil.6/- Kilakala

Mbunge aahidi kutoa mil.6/- Kilakala

Mbali na msaada huo wa Abood, uongozi wa kata hiyo chini ya Diwani, Ribbon Mkali, umeahidi kutoa mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi huo.

Mtaa wa Chalumbi umeanza baada ya wananchi kuchangia nguvu kazi ya thamani ya Sh milioni 3.3. Mbunge huyo alitoa ahadi hiyo juzi baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa vivuko hivyo kwenye mitaa.

Alisema vitarahisisha utoaji wa huduma za jamii. Mitaa hiyo ipo katika miinuko inayotenganishwa na mto Kilakala, hivyo kusababisha ugumu wa usafiri kwa njia ya baiskeli, pikipiki na magari.

Mbunge huyo aliwataka wananchi wa mitaa hiyo pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa na Kata, kusimamia fedha zinazotolewa na wadau na Halmashauri kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vivuko hivyo.

Ofisa Mtendaji wa Mitaa hiyo, Felista Sanga, alisema wananchi wa mtaa wa Nugutu, wamepanga kuchangia nguvu kazi ya thamani ya Sh milioni 3.8 na tayari wamekusanya Sh 50,000.

Katika hatua nyingine, Abood aliitaka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, kuondoa dampo la taka lililopo mtaa wa Mbuyuni Kata ya Mafisa kwa kuwa lipo jirani na makazi ya watu.

Alisema Halmashauri inapaswa kutafuta eneo jingine mbali na makazi ya watu, kwa lengo la kuwalinda na hatari ya magonjwa ya milipuko na sugu, ikiwemo saratani.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Daudi Salum alisema mtaa huo umekuwa na kero ya harufu mbaya ya takataka, inayotoka kwenye dampo na maji machafu ya viwandani ambayo yamekuwa na kemikali.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata hiyo , Francis Kayenzi , alisema tayari alishawasilisha kero hizo kwa Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa lakini hakuna juhudi zozote zilizofanywa ili kuziondoa kero hizo.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi