loader
Mbunge ahoji uwekezaji ATCL

Mbunge ahoji uwekezaji ATCL

Sanya aliuliza “Hivi karibuni tulisikia yupo Mwarabu kutoka Oman ambaye yupo tayari kuwekeza kiasi cha dola milioni mia moja kwa ajili ya kulifufua Shirika la Ndege la ATCL. Je, suala la mwekezaji huyo kutaka kuwekeza katika shirika hilo la ndege imefikia wapi?”

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema mazungumzo kati ya Serikali na wawekezaji mbalimbali, akiwemo mwekezaji kutoka Oman, yatakamilika baada ya mchakato wa kusafisha mizania ya ATCL utakapokamilika.

Mizania hiyo inahusisha madeni ya ATCL yanayofikia Sh bilioni 133, kuchukuliwa na Serikali na kuyawekea utaratibu maalumu wa kuyahakiki, kuyajadili na wadai na kuyalipa, huku ATCL ikianza upya shughuli zake bila mzigo wa madeni.

“Wizara ilishawasilisha serikalini Mpango Mkakati wa Kuifufua ATCL ambao uko hatua za mwisho kuridhiwa na vyombo husika,” alisema Tizeba.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi