loader
Miaka 30 kwa kumbaka mtoto

Miaka 30 kwa kumbaka mtoto

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Hassan Said alisema mshitakiwa ataanza kutumikia kifungo hicho atakapokamatwa kwani alitoroka alipopewa dhamana.

Alisema Mahakama imeamua kutoa hukumu hiyo pasipo mshitakiwa kuwepo mahakamani kwa kuwa kesi hiyo ni ya mwaka 2010, inataka kuachana nayo ili kuendelea na mashitaka mengine.

Kwa mujibu wa Hakimu, ushahidi wa mtoto aliyefanyiwa vitendo hivyo ulionesha kuwa alimfahamu mshitakiwa huyo tangu akiwa mdogo kwani alikuwa mlinzi wa shuleni kwao na jirani na nyumba yao.

Mshitakiwa alikuwa akimdanganya mtoto huyo aliyekuwa pamoja na rafiki yake kwa kuwapa Sh 100 ya kununulia Ice cream na kuwataka wasiseme kwa wazazi.

Anadaiwa kutenda kosa hilo, Septemba 24, mwaka 2010 maeneo ya Kitunda Kati , Wilaya ya Ilala. Mzazi wa mtoto huyo aligundua hali hiyo baada ya mtoto huyo kuchelewa kurudi nyumbani na kumhoji sababu.

Ingawa mshitakiwa alikana baada ya kusomewa mashitaka, Hakimu alisema kukimbia kwake, kumempotezea haki yake ya kujieleza.

Wakili wa Serikali Munde Mwakalombola alidai kutokana na kosa hilo adhabu itakayotolewa iwe fundisho kwa wanaume wanaofanya vitendo hivyo.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi