loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Michuano ya magongo yaanza Tanga

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania (TAHA), Kaushik Doshi alisema jana kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu tisa.

Doshi alizitaja timu hizo kuwa ni Polisi ya Kenya, TPDF ya Dar es Salaam, Tanzania Ladies 11, Moshi Khalsa, El Hilal ya Tanga, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mombasa Mwita na Kampala Klabu.

Alisema tayari timu zimepangwa kwenye makundi matatu ambapo kwa kila moja zipo timu tatu.

Kundi A kuna timu za Kenya Polisi, TPDF na Tanzania Ladies, Kundi B kuna Moshi Khalsa, El Hilal na Chuo Kiku cha DSM wakati Kundi C kuna Mombasa Mwita, Kampala klabu na Kili Vijana.

“Maandalizi yako vizuri, tutaanza mchana wa leo, tunashukuru kupata udhamini wa Phoenix Assurance, tunaahidi Watanzania timu zetu zitajitahidi kutokana na maandalizi ya muda mrefu,” alisema Doshi.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi