loader
Mjumbe Bunge Maalum alazwa

Mjumbe Bunge Maalum alazwa

Ziana alifikwa na hali hiyo leo asubuhi bungeni mjini Dodoma wakati wajumbe hao wakiendelea kuchangia mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba.

Wakati mjumbe mmoja akiendelea kutoa mchango wake ghafla Ziana aliangua kilio tukio lililozua taharuki na baadhi wa wajumbe wenzake kumfuata kumsaidia.

Wakati wajumbe hao wakimfuata baadhi ya wajumbe wenye taaluma ya udaktari akiwemo Dk David Mwakyusa walifika alipo mjumbe huyo kwa lengo la kumsaidia na hivyo kutoka naye nje ya ukumbi wa Bunge.

Muda mfupi baadaye, Mwenyekiti wa Bunge hilo alitoa taarifa na kusema mjumbe huyo amepokea taarifa ya msiba wa baba yake na yeye amepata mshtuko na amelazwa Hospitali ya Mkoa ya Dodoma.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi