loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mkulo mgeni rasmi Miss Kanda ya Mashariki leo

Mgeni rasmi kwenye kinyang’anyiro hicho anatarajiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mustafa Mkulo, na mshindi ataondoka na Sh 400,000 pamoja na cheti.

Mratibu wa shindano hilo, Alexander Nikitas, alisema jana mjini kuwa warembo hao ni kutoka mikoa minne inayounda kanda hiyo, na idadi yao kwenye mabano ni Morogoro (4), Lindi (2), Pwani (3) na Mtwara (3).

Aliwataja kwa majina kuwa ni Lucy Diyu, Prisca Mengi, Angel Shio na Alicia Shayo (Morogoro), Leila Abdul na Elizabeth Eliud (Lindi), Nidah Katunzi, Mellabol Emanuel na Lightness Mziray (Mtwara) wakati kutoka Pwani ni Khadija Sihaba, Faith Msuya na Mary Mpelo.

Mbali na kutaja majina yao na zawadi ya mshindi wa kwanza, alisema mshindi wa pili atapewa Sh 300,000, wa tatu Sh 200,000 na wa nne Sh 150,000. Wengine watapewa kifuta jasho cha Sh 100,000 kila moja.

Warembo watakaoshika nafasi nne za juu watapata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Pia alisema katika kinyang’anyiro hicho kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa kundi la taarabu la Jahazi likiongozwa na Mzee Yusuph, Wanne Star na mwanamuziki maarufu wa hip hop, Kala Jeremiah.

Shindano hilo la mrembo wa Kanda ya Mashariki linadhaminiwa na kampuni mbalimbali zikiwemo Redd’s, Pepsi, Clouds FM, Jambo Leo, Father Kidevu Blog na Michuzi Blog.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi