loader
Msanii wa India akonga nyoyo Dar

Msanii wa India akonga nyoyo Dar

Onesho hilo lilifanyika katika Kituo cha Utamaduni cha India, ikiwa ni katika kusherehekea miaka 68 ya Uhuru wa India.

Madhav, ambaye ni mahiri katika miondoko ya asili ya Odissi, alionesha umahiri wake kwa kucheza nyimbo kadhaa ambazo ziliwavutia watu waliofika kushuhudia onesho hilo.

Msanii huyo aliongozana na wasanii wenzake ambao ni wapiga ala za asili, Satya Katha, Prafulla Kumar Mangaraj na Dhiraj Pandey.

Balozi wa India nchini, Debnath Shaw alisema katika mwendelezo wa kusherehekea Uhuru wa nchi yao, wanatarajia kuwaleta wasanii wengine kufanya onesho nchini.

Onesho hilo limepangwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha India, Chitra Suresh alisema mbali ya onesho la Dar es Salaam, Madhav pia atafanya onesho Zanzibar.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi