loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mtibwa Sugar kamili kuivaa Azam FC

Mtibwa Sugar kamili kuivaa Azam FC

Akizungumza na gazeti hili jana, Maxime alisema tangu wameanza mazoezi ya kujifua hii ni wiki ya pili na wanategemea mechi hiyo itawapa changamoto ya kujiandaa kuelekea kwenye msimu mpya.

“Ndio kwanza hii wiki ya pili tangu tuanze mazoezi, lakini kikosi chetu kinaendelea kujifua, tukitegemea kupata ushindi wa mechi hiyo, ikiwa pia ni sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu mpya,” alisema kocha huyo ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo na timu ya Taifa, Taifa Stars.

Kikosi cha wachezaji 26 wa zamani na wapya kimekuwa kikifanya mazoezi kwenye uwanja wa bora tayari kwa maandalizi sio tu kuelekea kwenye mechi ya kirafiki, bali kujiimarisha zaidi ili kuanza Ligi Kuu kwa kasi.

Mexime alisema katika kikosi chake kilichojaa wachezaji wengi wa Kitanzania, ana imani mwaka huu watacheza Ligi ya kiushindani kutokana na kuanza maandalizi mapema.

Alisema malengo yao ni kuhakikisha msimu huu wanafanya vizuri na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu. Mtibwa Sugar hivi karibuni walifanya usajili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Miongoni mwa wachezaji hao ni beki wa kulia, Majaliwa Shaban kutoka JKT Oljoro iliyoshuka daraja msimu uliopita. Aidha, imewapandisha vijana watatu ambao ni Hassan Mmbande, Patrick Athanas na Makarani.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi