loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mtoto afa kwenye shimo la choo

Mtoto afa kwenye shimo la choo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema maiti ya mtoto huyo alikutwa juzi saa 11 jioni maeneo ya Ulongoni 'B', ikiwa kwenye shimo hilo ambalo halijaanza kutumika.

Maiti ya mtoto huyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hakuna aliyekamatwa na upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

Katika tukio jingine, mtembea kwa miguu asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 25 amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari akivuka barabara.

Kamanda Minangi alisema ajali hiyo ni ya juzi saa 3 usiku katika barabara ya Kawawa eneo la Kigogo Sambusa, gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na mtu asiyefahamika akitoka Msimbazi Center kwenda Kigogo lilimgonga mtu huyo na kusababisha kifo chake.

Maiti amehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na juhudi za kulitafuta gari na dereva aliyekimbia baada ya ajali zinaendelea.

Katika tukio la tatu, mwanamume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 35 amekufa baada ya kugongwa na pikipiki aina ya Fekon yenye namba T793 CSW iliyokuwa ikiendeshwa na mtu asiyefahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema ajali hiyo ni ya juzi saa 10 jioni katika Barabara ya Kilwa eneo la Mto Kizinga darajani.

Alisema mwendesha pikipiki huyo akitoka Mtongani kwenda Mbagala Mission alimgonga mtembea kwa miguu huyo. Maiti amehifadhiwa Hospitali ya Temeke na pikipiki imehifadhiwa Kituo cha Polisi na juhudi za kumtafuta mtu huyo aliyekimbia zinaendelea.

Katika tukio jingine, Kamanda Kiondo alisema, mtembea kwa miguu asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 amekufa baada ya kugongwa na gari lisilofahamika.

Alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 2 usiku katika Barabara ya Kilwa eneo la Sabasaba kwa Mpili, ambapo gari hilo likiendeshwa na mtu asiyefahamika akitoka Mbagala kwenda Mtongani alimgonga mtu huyo na kusababisha kifo chake.

Maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke, juhudi za kulitafuta gari na dereva aliyekimbia baada ya ajali zinaendelea.

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi