loader
Mtumishi Ikulu afa uwanjani Mei Mosi

Mtumishi Ikulu afa uwanjani Mei Mosi

Mkasa huyo ulitokea majira ya asubuhi katika Uwanja wa Taifa wa Uhuru ambapo mamia ya wafanyakazi wa mkoa huo, walijikusanya kwa ajili ya maandamano ambapo mtumishi huyo alikuwa ni mmoja wa watumishi wa Ikulu waliokuwepo kwenye maandamano hayo.

Dakika chache kabla ya kuwasili kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi uwanjani hapo, shamrashamra zilizotawala viwanjani hapo, zilizimwa na sauti ya honi za gari dogo lililokuwa likimkimbikiza mtumishi huyo kupatiwa huduma ya kwanza iliyokuwa ikitolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Kwa mujibu wa wafanyakazi wenzake, walioomba kutotajwa majina yao, Chilwangwa aliyekuwa na matatizo ya ugonjwa wa kisukari, asubuhi ya jana alijiunga na wenzake kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo, na walipofika uwanjani hapo, aliaga anakwenda msalani.

Baada ya kufika msalani inadaiwa alianguka ghafla, na watoa huduma za afya ambao ni Shirika la Msalaba Mwekundu walijitahidi kumpatia huduma ya kwanza bila mafanikio na alipoteza maisha akiwa uwanjani hapo.

MSANII wa Filamu nchini, Isarito Mwakalindile, maarufu kama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi