loader
Mume wa Flora Mbasha kizimbani

Mume wa Flora Mbasha kizimbani

Mshitakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji, alipanda kizimbani jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai Mei 23 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga Wilaya ya Ilala mshitakiwa alitenda makosa mawili.

Katika shitaka la kwanza, anadaiwa maeneo ya Tabata Kimanga wilayani Ilala, alimbaka shemeji yake. Katuga alidai Mei 25 mwaka huu, maeneo ya Tabata Kimanga, alimbaka tena mfanyakazi wake wa ndani.

Mshitakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

Alitakiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka taasisi za Serikali watakaosaini kulipa Sh milioni tano. Kesi itatajwa Juni 19 mwaka huu.

Vituo vya afya vyafikia 8461Idadi ya Vituo vya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi