loader
Mwekezaji apiga jeki wakulima wa mpunga

Mwekezaji apiga jeki wakulima wa mpunga

Wakulima hao wa Kijiji cha Mgeta wilayani Morogoro, wananufaika kwa kupewa mbegu, kupaliliwa mashamba yao na kupewa elimu kwa ajili ya kuvuna mazao mengi zaidi ili waweze kujikimu.

Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Chris Maongezi alisema pia wananchi hao wanasaidiwa kuuza mazao yao kwa urahisi, kutokana na kuwauzia wao.

“Huu ni mradi maalumu ambao unasaidia familia takribani 6,500 kila upande uliotuzunguka, tunawasaidia wakimaliza kuvuna, tunayanunua mazao yao,” alisema Maongezi.

Alisema pia shamba hilo limetoa ajira za kudumu kwa watu 250, huku wakati mavuno ajira ndani ya shamba hilo hufikia 400. Alisema ili familia ziweze kunufaika na mradi huo ni lazima zijiandikishe.

Alisema kufanya hivyo, kunawasaidia wakulima kujikimu na kunufaika na kilimo wanachofanya

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko na Katuma Masamba

Post your comments