loader
Nagu: Wekezeni walipo wananchi

Nagu: Wekezeni walipo wananchi

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Jamhuri ya Czech.

Alisema uchumi wa Tanzania unakua kwa haraka ambapo kwa sasa umefikia asilimia saba ambayo ni dalili ambayo ilitakiwa wananchi wawe wameondokana na umasikini lakini kutokana na kutowekeza katika eneo ambalo ndipo walipo wananchi wengi ukuaji huo hauwezi kuonekana.

“Tutumie fursa ya kukuta na wawekezaji kama hawa kwa ajili ya kuwekeza katika maeneo ambayo wananchi walio wengi ndipo walipo,” alisema Dk Nagu na kuongeza maeneo hayo kuwa ni katika kilimo ambapo ndipo penye mchango mkubwa wa kukua kwa uchumi.

Alisema ni wakati muafaka kuwavutia wawekezaji kwani wana mitaji ambayo italeta manufaa kwa wananchi kwa kuhakikisha wanaongeza ajira pamoja na teknolojia.

Dk Nagu alisema sekta ya viwanda ni moja ya eneo ambalo hukua kwa kasi Afrika, ambapo Tanzania ina vivutio kadha wa kadha pamoja na rasilimali mbalimbali ambazo zinaweza kutumika viwandani.

“Kutokana na kuwepo kwa rasilimali nyingi nchini inawahakikishia wawekezaji kuwa na malighafi za kutosha kwa ajili ya kuendeshea katika viwanda,” alisema Dk Nagu na kuongeza kuwa tayari yamefanyika mapitio katika sera na sheria katika sekta ya nishati inayolenga kuruhusu sekta binafsi kushiriki katika kuzalisha, kusambaza na kugawa.

Kwa upande wake, Mkuu wa ujumbe kutoka Czech, Pavel Rezak alisema Jamhuri ya Czech kwa kushirikiana na Tanzania zitaendelea kuimarisha uchumi wa nchi hizo kutokana na ushirikiano wa muda mrefu uliopo.

Alisema kupitia mkutano huo hautojikita kwa kutazama kukuza uchumi na biashara pekee kati ya nchi hizo lakini pia kuwa mkombozi wa kuimarisha manufaa kwa pande zote.

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi