loader
Naibu Waziri 'amalizana' na Balozi

Naibu Waziri 'amalizana' na Balozi

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema hayo jana alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo, aliyetaka Serikali itoe tamko kuhusu ulipofikia mgogoro huo.

Lyimo katika hoja yake, aliyoitoa baada ya kuomba muongozo wa Spika, alisema kwa kuwa Maselle alimtuhumu Balozi huyo wa Uingereza bungeni, ingekuwa vyema hatua za Serikali za kumaliza mgogoro huo, zitolewe taarifa bungeni.

Kwa mujibu wa madai ya Lyimo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametoa taarifa kuwa tuhuma za Maselle zilikuwa uzushi na amenukuliwa katika vyombo vya habari.

Lyimo alidai kwa kuwa Uingereza imekuwa ikitoa misaada mingi nchini na kwa kuwa tuhuma hizo zilitokea bungeni, ni sahihi kwa Serikali kutoka kauli yake kuhusu kilichoafikiwa.

Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri Mkuu Pinda alisema baada ya kusikia suala hilo, aliona kiutaratibu lilipaswa kupelekwa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Alifafanua kuwa alimwagiza Waziri Membe alishughulikie, ambapo taarifa alizonazo, aliwakutanisha Maselle na Balozi Melrose wakazungumza na kuelewana.

“Hakuna haja ya kuliendeleza hili wakati hawa walishaelewana,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Maselle wakati wa kujadili na kutoa majibu kuhusu Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, aliripotiwa akisema kuna ripoti kwamba Balozi wa Uingereza amekuwa akijihusisha kuratibu vikao mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma kinyume cha utaratibu na hadhi ya kidiplomasia.

Baada ya hapo kulijitokeza taarifa mbalimbali zilizopingana na madai hayo ya Maselle, ambapo jana Pinda alifafanua kuwa Naibu Waziri huyo na Balozi huyo, waliitwa katika kikao na kumaliza tofauti kidiplomasia.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi