loader
Ni kosa la jinai kwa ofisa wa serikali kuongopa Barazani

Ni kosa la jinai kwa ofisa wa serikali kuongopa Barazani

Mzee alisema hayo wakati alipowasilisha mada ya wajibu na utekelezaji kazi za makatibu wa kamati za Baraza hilo mkoani Kusini Unguja.

Akifafanua aliseka kifungu cha 22 cha Sheria ya Baraza la Wawakilishi namba nne ya mwaka 2007 inayohusu kinga na fursa, inakataza mtu kuidanganya Kamati ya Baraza la Wawakilishi wakati inapotekeleza majukumu yake.

Alisema mtu atakayebainika kwa makusudi kutenda kosa hilo ataadhibiwa kwa mujibu washeria za makosa ya jinai. Mzee alisema kamati za Baraza hilo zina uhalali wa kikatiba na sheria kwa hivyo si vyema kwa maofisa wa umma kutoa majibu au ushahidi wa uongo.

“Nataka nibainishe kwamba kamati za Baraza la Wawakilishi zipo kwa mujibu wa Katiba kwa hivyo zinapotekeleza majukumu yake zinafanya kazi kwa maslahi ya wananchi kwa hivyo watendaji wa umma wanatakiwa kutoa mashirikiano yao dhati,” alisema Mzee.

Aidha Mzee ambaye alipata kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa zaidi ya miaka mitano alisema ni haki kwa wajumbe wa kamati ya baraza hilo kupata taarifa wanazozitaka kutoka kwa watendaji wa Serikali tena kwa usahihi.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi