loader
‘Ni ruksa kujenga matuta barabarani’

‘Ni ruksa kujenga matuta barabarani’

Amesema madereva hawaheshimu ukomo wa mwendokasi, na kama wataendelea kukaidi kutekeleza sheria za usalama barabarani, ukubwa wa matuta uongezwe.

“Walipo watu wekeni matuta wapunguze mwendo…weka tuta, watalalamika lakini maisha ya watu yamenusurika,” alisema Rais Kikwete muda mfupi kabla ya kufungua barabara ya Songea- Namtumbo, na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Namtumbo- Kilimasera- Matemanga.

“Kwa sababu wapo hivyo wekeni matuta tu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kwamba, madereva nchini hawaheshimu kipimo cha mwendokasi. “Madereva muendeshe kwa uangalifu, mheshimu ukomo wa mwendo,” alisema Rais Kikwete na kutaka madereva pia waheshimu masharti ya uzito wa mizigo barabarani, na wananchi nao waitunze miundombinu hiyo.

“Kwa hiyo sharti langu, ombi langu, barabara hii muitunze, kwanza kuitunza, wenye magari wazingatie masharti ya uzito kwenye barabara,” alisema Rais Kikwete kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, wawakilishi wa Benki ya Maendeleo Afrika, wawakilishi wa balozi za Marekani na Japan, na viongozi wa Serikali wakiwemo mawaziri.

“Msifanye barabara mahali pa kupitishia ng’ombe, kwato za ng’ombe zinaharibu barabara…kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake,” alisema Rais Kikwete.

Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa alimshukuru Rais Kikwete kwa kutekeleza ahadi kwa wananchi kuwajengea barabara na kuwapatia fedha za kujenga hospitali ya wilaya aliyoifungua baada ya kufungua barabara hiyo.

“Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana, kwa niaba ya wananchi wa Namtumbo tunasema asante… Mungu akujalie afya njema, akupe umri mrefu, eeh Mwenyezi Mungu mjalie Rais wetu,” alisema Kawawa.

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema kwenye mkutano huo kuwa, kufunguliwa kwa barabara hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Rais Kikwete.

Alishukuru Mfuko wa Maendeleo wa Milenia (MCC) kwa kuwezesha kujengwa kwake kwa gharama ya Sh bilioni 97.7.

“Watu wa Namtumbo wameona lami, hakuna aliyekuwa na ndoto hiyo ndiyo maana wamejiita Namtumbo kwa sababu vitu vya tumboni huwa havionekani lakini lami tumeiona,” alisema Waziri Magufuli.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments