loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nidhamu itawale Michezo ya Feasssa

Nidhamu itawale Michezo ya Feasssa

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuandaa mashindano hayo, ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2006, huku shule ya Makongo ikiwa mratibu mkubwa wa mashindano hayo.

Mwaka huu, mashindano hayo yanatazamiwa kuwa na msisimko zaidi kwani yanaandaliwa kitaifa zaidi tofauti na mwaka 2006 ambako Shule ya Sekondari ya Makongo ndio ilikuwa mstari wa mbele kuyaandaa nchini.

Ni matarajio yangu kuwa timu za shule za Tanzania zitakuwa zimejiandaa vizuri ili kuhakikisha mataji mengi yanabaki nyumbani. Watanzania hawajasahau timu ya Tanzania iliyoshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola iliporudi mikono mitupu, licha ya ahadi waliyotoa mbele ya kiongozi wa nchi, Rais Jakaya Kikwete pale kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Michezo hiyo ya Feasssa pamoja na kuanza leo, lakini itazinduliwa rasmi kesho na Rais Kikwete, hivyo ni matarajio ya wengi kuwa, shule zetu hazitarudia makosa yaliyofanywa na timu ya Michezo ya Madola kurudi bila medali.

Katika michezo hiyo kutakuwa na michezo mingi kama soka, mpira wa meza, tenisi (lawn tennis), rugby, mpira wa magongo, mpira wa kikapu, netiboli, mpira wa wavu, badminton na mingine.

Mbali na wenyeji Tanzania, nchi zingine zinazotarajia kuleta shule zao ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

Ni matarajio ya wengi kuwa baada ya maandalizi ya muda mrefu na kufanya mashindano ya mchujo ili kupata shule zitakazowakilisha nchi katika michezo hiyo, ni matumaini yetu kuwa shule zetu kamwe hazitakuwa sawa na kichwa cha mwenda wazimu.

Mashindano hayo yanasaidia kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanafunzi wa nchi za Afrika Mashariki na kuinua vipaji vya vijana katika michezo mbalimbali.

Pia ni sehemu ya mafunzo kwa vijana wetu kujifunza kutoka kwa wenzao na wenzao kujifunza kutoka kwa wanafunzi wa Tanzania kuhusu michezo fulani.

Mfano katika riadha, hakuna ubishi kuwa wanafunzi wa Tanzania watakuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa Kenya ambao ni mahiri katika mchezo huo duniani.

Nidhamu pia ni kitu kingine muhimu sana katika michezo na hatutarajii kusikia kuwa wanafunzi wetu wameonesha tabia mbaya mbele ya viongozi au wachezaji wenzao wa nchi zingine, hilo kamwe halitakubalika.

Michezo bila nidhamu hakuna mafanikio, hivyo tunatarajia tutaona nidhamu kutoka kwa wachezaji wetu na kufanya vizuri katika michezo yote watakayoshiriki.

Tunachotaka kuona katika michezo hiyo ya Feasssa ni nidhamu kutoka kwa wachezaji, waamuzi, mashabiki, viongozi na wadau wengine wa michezo ili kuhakikisha mshindi anapatikana kwa haki na mashindano yamalizika salama.

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi