loader
NSSF yakopesha bil. 1.5/- Singida

NSSF yakopesha bil. 1.5/- Singida

Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Magreth Mwaipeta aliyasema hayo juzi wakati wa semina kwa viongozi wa kikundi cha wachimbaji wa madini ya dhahabu cha Aminika Gold Mines cha Sambaru wilayani Ikungi.

Alivitaja vikundi vilivyofaidika na mikopo hiyo kuwa ni VETA Singida (Sh milioni 500), Mtinko (Sh milioni 164), Amani Manyoni ( Sh milioni 223), Kumekucha - Itigi (Sh milioni 50), Tumaini Singida (Sh milioni 89) na Ndago – Iramba ( Sh milioni 500).

Mwaipeta alisema kuwa mikopo hiyo ilitolewa kwa riba nafuu kwa vikundi hivyo sita wanachama wake waweze kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa vikundi hivyo vilipata mikopo hiyo baada ya kukidhi vigezo vya Shirika hilo, ikiwa ni pamoja na kuwa na amana za Chama asilimia hamsini; na kwamba kiwango cha chini kukopa ni Sh milioni 50 wakati kiwango cha juu ni shilingi bilioni moja tu.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Singida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi