loader
Dstv Habarileo  Mobile
Nyota wa Bondeni wamtakia heri Muhando

Nyota wa Bondeni wamtakia heri Muhando

Rose Muhando atazindua albamu yake hiyo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Muhando alisema wanamuziki Solly Mahlangu, Rebecca Malope na Sipho Makabane, wamemtakia kila la heri katika uzinduzi huo kwa kuwa wamekuwa wakishirikiana mara kwa mara katika shughuli za muziki huo ndani na nje ya nchi.

“Solly Mahlangu, Rebecca na Makabane wamenitumia salamu za kunitakia heri katika uzinduzi wangu wa albamu Jumapili. Unajua hawa tumekuwa tukishirikiana nao katika shughuli za muziki ndani na nje ya nchi. Mara kwa mara wamekuwa wakija hapa nchini katika matamasha mbalimbali ambayo mimi pia nimekuwa nikialikwa,” alisema Muhando.

Alisema anaamini salamu hizo zitakuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha uzinduzi huo kwani hao wamekuwa na mchango mzuri katika uimbaji wa nyimbo za Injili.

Uzinduzi huo wa albamu ya Kamata Pindo la Yesu ya Rose Muhando baada ya jijini Dar es Salaam, unatarajia kuendelea katika mikoa ya Tabora na Geita. Baada ya uzinduzi huo wa Dar es Salaam, utahamia mikoa ya Tabora na Geita.

Agosti 8 itakuwa zamu ya mashabiki wa muziki wa Injili mkoani Tabora, Geita itakuwa Agosti 9 na Agosti 10 jijini Mwanza. Uzinduzi huo wa video hiyo umefanikishwa na Kampuni ya Msama Video Productions ya Dar es Salaam.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi