loader
Pinda awataka wadau kusaidia walima pamba

Pinda awataka wadau kusaidia walima pamba

Pinda aliyasema hayo juzi alipokuwa akifunga Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yaliyofanyika katika viwaja vya Nyamhong’oro, nje kidogo ya jiji la Mwanza ambapo halmashauri 41 za mikoa ya Kanda ya Ziwa zilishiriki.

Alisema katika kilimo cha pamba changamoto kubwa ni mbegu za manyoya na zile ambazo hazina manyoya na kuuzwa kwa bei ya chini ambayo inampumbaza mkulima wakati hazina tija katika kilimo hicho.

Alisema kinachotakiwa ni wadau hao kuandaa mashamba darasa ambayo yatatoa taswira ya mbegu bora kwa mkulima na kumuacha afanye maamuzi ya mbegu ipi atumie.

“Nimetembelea mashamba darasa nimeona jinsi ambavyo pamba iliyopandwa kwa kutumia mbegu zisizo na manyoya zinavyoota na nimepata maelezo kutoka kwa mkulima kuwa kwa kutumia mbegu hizo ekari mmoja inatoa kilo 1,500,” alisema.

Alisema kuwa tatizo linajitokeza kwa sababu mzalishaji wa mbegu hizo nchini ni mmoja na kufanya watu wawe na hisia tofauti.

“Nawaagiza wakuu wa mikoa akitokea mtu mwigine ambaye anazalisha mbegu zenye tija aruhusiwe, ila kumbukeni hata sisi tunahitaji kuuza mbegu hizo nje, wekezeni katika kilimo cha pamba ili kutoa ushindani na muache wivu,” alisema.

Pinda alitaja changamoto nyingine katika kilimo cha pamba kuwa ni kilimo cha mkataba na kuwaagiza viongozi wa mkoa na halmashauri kama wana uwezo wawapatie wakulima pembejeo.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Grace Chilongola, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi