loader
Pinda: Viwanja vya Sabasaba vyatakiwa kujengwa upya

Pinda: Viwanja vya Sabasaba vyatakiwa kujengwa upya

Amesema umefika wakati eneo hilo, Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, linapaswa kubomolewa na kujengwa upya na kisasa.

Pinda alisema pamoja na kuongezeka kwa mataifa makubwa kushiriki katika maonesho hayo, lakini eneo la maonesho halina mvuto wa kimataifa.

Alisema ni vema kusimamisha maonesho hayo hata kwa mwaka mmoja ili kuvunja majengo yote na kujenga upya kwa kutumia taasisi za ndani kama Benki ya Uwekezaji (TIB) au Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwani kwa fedha za ndani inawezekana kuleta mvuto.

“Lazima kufanya uamuzi sasa wa kubomoa uwanja huu na kujenga upya hata ikibidi kusimama maonesho kwa mwaka mmoja na kujenga kwani hata njia za kupita ni finyu za tokea zamani lazima kubadilishana kuwa na wakati kama maonesho yalivyo,” alisema Pinda katika ziara yake ya saa mbili, alitembelea mabanda mbalimbali yakiwemo, Banda la Asali, Banda la Kampuni ya Property International, TIB, Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Tanzania (VETA) na Banda la Tanzania.

Katika hatua nyingine, alisema sekta binafsi ina uwezo wa kufanya mambo mazuri katika kukuza uchumi.

Alitoa mfano wa Chuo cha Global Link Education kinachounganisha wanafunzi kusoma nje ya nchi, zaidi kwenye vyuo vinavyotambulika, hivyo kuondoa changamoto ya vijana kurudi na vyeti vya nje ya nchi visivyo na ubora.

Pinda alisema chuo hicho kimesaidia kuondoa urasimu uliopo serikalini katika kushughulikia ufadhili nje ya nchi kwa kutoza gharama ndogo, huku wakieleza kwa uwazi nafasi na nchi zenye vyuo vizuri vya taaluma mbalimbali.

Waziri Mkuu alieleza pia kufurahishwa na benki za NMB na TIB kusaidia wajasiriamali wadogo. Kwa mujibu wake, NMB pekee imesaidia Sh bilioni 50 jambo ambalo ni mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi.

Aliomba benki zote nchini kungalia namna ya kukuza mradi huo wa kusaidia wafanyabiashara wadogo nchi nzima ikiwemo ukopeshaji wa baiskeli za miguu mitatu yaani bajaj na pikipiki huku wakiwapatia mafunzo kwanza kuepuka ajali.

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi