loader
Dstv Habarileo  Mobile
Polisi, bodaboda wajibikeni kuokoa maisha

Polisi, bodaboda wajibikeni kuokoa maisha

Awali, pikipiki zilionekana kuwa mkombozi kwa maana ya kurahisisha usafiri, ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama, kupunguza adha kwa abiria hasa kukiwa na foleni, kumwahisha abiria afike haraka anapokwenda, na kupunguza ukubwa wa tatizo la ajira hasa kwa vijana, lakini sasa kwa wengi bodaboda ni ‘majanga’.

Watu wengi wanapoteza maisha na wengine kupata ulemavu katika ajali za bodaboda si kwa kuwa Mungu amepanga, ni kwa sababu ya uzembe, sifa za kijinga, na makosa mengine ya madereva wakiwemo wa magari, wa baiskeli na hata watembea kwa miguu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, madereva 870 wa bodaboda na abiria 228 walikufa kutokana na ajali 8,241 za barabarani mwaka jana, hivyo kwa ujumla pikipiki hizo ziliua watu 1,098 nchini, na 6,578 walijeruhiwa.

Ajali hizo za bodaboda zilijeruhi madereva 5,237 vya vyombo hivyo vya usafiri na kwa kuzingatia kauli ya Rais Jakaya Kikwete, ajali za pikipiki ni nyingi kuliko za magari.

Hivi karibuni, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani, Mohamed Mpinga alisema, ajali za bodaboda zimeongezeka kwa asilimia 18.5 ikilinganishwa na matukio 5,763 yaliyotokea mwaka juzi.

Kwa kuzingatia kasi ya sasa ya ajali hizo, Rais Jakaya Kikwete hajakosea kusema kuwa, kama kasi ya ajali za pikipiki itaendelea kama ilivyo sasa, utafika wakati idadi ya watu watakaokufa kwa ajali hizo itakuwa kubwa kuliko wakaopoteza maisha kutokana na upungufu wa kinga mwilini (Ukimwi).

Kauli hii ya mkuu wa nchi ni nzito si tu kwa kuonesha ukubwa wa tatizo, lakini kwa sababu pia inatoa changamoto kwa jamii kujiuliza kama kweli bodaboda ni mkombozi au adui wa uhai na ustawi wa wananchi wanaoathiriwa na ajali hizo.

Julai 19 mwaka huu, wakati akiwa mjini Mbinga, Rais Kikwete aliwaagiza Polisi wahakikishe madereva wa pikipiki na abiria wao wanavaa kofia ngumu ili kuepuka madhara makubwa zinapotokea ajali.

Kwa kiasi kikubwa, polisi hawajatekeleza agizo hilo, abiria wengi kwenye pikipiki hawavai kofia hizo, na polisi wanawaona.

Rais alisema, sharti la watu kuvaa kofia ngumu si la urembo, Polisi wanapaswa kuipa uzito unaostahili kauli hii kwa kuwaadhibu madereva wa bodaboda wanaokiuka sharti hilo ili kuokoa maisha ya wananchi.

Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, ametoa agizo kwa Polisi, kwa nini hawatekelezi? Kama Polisi hawaheshimu amri ya Rais, wataiheshimu ya nani?

Kama wameshindwa kutekeleza amri hiyo wamwambie aliyeitoa ili awaagize wengine kwa sababu kila siku wananchi wanatumia usafiri wa pikipiki.

Madereva wa bodaboda timizeni wajibu wenu, usalama wa abiria wenu ni muhimu kama ulivyo wenu, na ikibidi, abiria anayekataa kuvaa kofia ngumu naye aadhibiwe kwa sababu anakiuka sharti halali la usalama barabarani.

Rais Kikwete amewataka Polisi msiwe walegevu katika kuhakikisha abiria wanavaa kofia ngumu, tangu kauli hiyo ilipotolewa, trafiki mlipaswa kuonesha ninyi si walegevu, lakini kwa kuwa bado madereva na abiria wanakiuka sharti hilo jamii huenda itashawishika kuamini kuwa Rais hakukosea, nyie lazima ni walegevu.

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi