loader
Polisi kizimbani wizi wa mtoto

Polisi kizimbani wizi wa mtoto

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Mbeya Maria Batulaine, Mwendesha mashtaka wa Serikali Juliana William, alisema washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na makosa mawili waliyoyatenda Aprili 4, mwaka huu huko wilayani Kyela.

William alisema kosa la kwanza la washitakiwa hao ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa la kuiba mtoto kosa ambalo wanatuhumiwa kulitenda Aprili 4, Mwaka huu, katika eneo la Songwe wilayani Kyela na kosa la pili kuwa ni la wizi wa mtoto.

Mwendesha mashtaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja mnamo Aprili 6, Mwaka huu katika eneo la Zahanati ya Njisi, Wilaya ya Kyela kwa makusudi waliiba mtoto mwenye umri wa siku saba kutoka kwa mama yake mzazi Mboka Mwakikagile.

Washtakiwa walikana kuhusika na tukio hilo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na upo tayari kuwaleta mashahidi wake kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi.

Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 6 Mwaka huu, na kwamba dhamana kwa washtakiwa iko wazi kama watakidhi vigezo ambavyo ni kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika zenye thamani ya Sh milioni 5, barua ya mtendaji na barua kutoka kwa mwajiri kwa ajili ya mshtakiwa wa kwanza.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi