loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

POROJO ZA ANKO SAGATI: Wamefeli mitihani, kisa ushirikiana!

Nasikia wafanyabiashara, wanasiasa ndio wanaoongoza katika kuwatumia washirikana kwenye shughuli zao. kama unataka ubunge unaambiwa huwezi kuingia hivi hivi ni lazima ukaandaliwe na wazee wa kazi.

Kwa sababu za kishirikiana, wanasiasa walihusishwa kushiriki kuwakata ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi viungo vyao. Jambo hilo likafanya ndugu zetu hao albino kuishi kwa wasiwasi na wengine kuhama majumbani kwao.

Mfanyabiashara anaamini kwamba ili watu wavutike kwenye biashara zake, lazima apate dawa ya mvuto. Wengine nasikia hata zana za kufanyia kazi kama ni mama lishe hata ule mwiko wake unaweza kukuta ni kiganja cha mtoto mchanga.

Wasomi wetu pia wamevutika kwenye kuamini ushirikina, wengi wetu ambao tumetoka maeneo ya vijijini huko, tumeshindwa hata kupaendeleza kwa kuogopa kurogwa. Kurogwa kumefanya huko tunakotoka tukususe kabisa.

Wengine wanashindwa hata kwenda likizo huko makwao kwa kuwa wanaamini kwamba wakienda huko wanaweza kuuawa. Sasa kwa kuwa ushirikiana ni moja ya imani zetu Waafrika, jambo hilo siku moja likaibuka na kulazimika kujadiliwa kwenye mkutano tena wa wadau wa elimu huko kwenye mkoa mpya wa Songwe.

Kumbe ni ushirikina ndio ambao baadhi ya shule za sekondari na msingi mkoani humo kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa. Bosi wa wilaya hiyo ndiyo iliyeibua jambo na kuuleza mkutano huo kuwa baadhi ya shule zilizoko kwenye eneo lake eti hazifanyi vizuri kwenye mitihani ya kitaifa kutokana na vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa wanafunzi.

Bosi huyo hakumng’unya maneno, alisema baadhi ya shule kwenye halmashauri yake vilitokea vitendo vya kuanguka na kupoteza fahamu wanafunzi siku chache kabla ya kufanyika kwa mitihani ya kitaifa mwaka jana.

Akasisitiza kuwa vitendo hivyo vya watoto kuanguka wakazi wa maeneo husika walivihusisha na imani za kishirikina kuwa vililenga kufifisha maendeleo ya watoto wanaosoma shuleni hapo.

Hebu mfuatilie hapa aliavyosema bosi huyo “Siku chache tu kabla ya mtihani unapokea taarifa kuwa watoto wa darasa la saba au kidato cha nne katika shule fulani wanaanguka na kuzirai. Cha ajabu yeye mwenyewe anasema haamini kwenye uchawi, lakini anapoenda

HAKUNA siri kila mtu anatamani sura nzuri na rangi isiyo ...

foto
Mwandishi: Shadrack Sagati

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi