loader
Dstv Habarileo  Mobile
Profesa Kikula aonya wahitimu UDOM

Profesa Kikula aonya wahitimu UDOM

Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula, alipozungumza na wanafunzi wa chuo hicho kwenye ufunguzi wa shirika linalojihusisha na kilimo na mazingira (Dreas) chuoni hapo.

Profesa Kikula alisema vijana wengi wasomi nchini, wamekuwa na tabia ya kupenda kuajiriwa bila kutambua kuwa wanaweza kutumia elimu yao kuanzisha ajira ambazo pia zitawasaidia vijana wengine.

Akizungumzia kuanzishwa kwa shirika hilo chuoni hapo, Kikula alisema kuwa uongozi wake umelipokea kwa mikono miwili na kutaka wanafunzi wengine kuiga mfano huo katika kubuni vitu vitakavyowapa ajira.

“Kuanzishwa kwa shirika hili kutakuwa kumewasaidia vijana kuendesha shughuli zao za kilimo na utunzaji wa mazingira lakini kubwa kabisa ni vijana kujiajiri wenyewe katika sekta ya kilimo,” alisema Kikula.

Mwenyekiti wa Dreas, Ally Bakari alisema pamoja na kuanzisha shirika hilo la kilimo na mazingira, bado wanakabiliwa na changamoto ya ardhi, fedha, wadhamini pamoja na vitendea kazi.

Bakari alisema shirika hilo, linajumuisha vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini ambao pia ni wanataaluma tofauti.

Vyuo hivyo ni pamoja na UDOM, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi