loader
Dstv Habarileo  Mobile
PSPF, TPB kukopesha wastaafu

PSPF, TPB kukopesha wastaafu

Mpango huo unaojulikana kama ‘Wastaafu Loan’ umelenga kukidhi mahitaji halisi ya fedha kwa wastaafu kwa mikopo ya gharama za matibabu, ada za shule, kuendesha biashara na miradi mbalimbali.

Akizungumza jana jijini wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu alisema utafiti walioufanya unaonesha kuwa wastaafu wanaingiza kiasi kikubwa cha fedha katika uchumi kutokana na mafao wanayolipwa ambayo kama watawekewa mfumo mzuri wanaweza kuleta athari chanya kiuchumi.

“Wazee wanaweza kuchangia katika uchumi kama vile kuongeza uwezo wa kifedha katika taasisi za kifedha, kuongeza ajira, kukuza kipato, kupunguza umasikini na kudumisha utulivu wa kisiasa.

“Kwa miaka minane mifuko ya jamii imeingiza katika mzunguko wa fedha kiasi cha Sh trilioni 2.6 kutokana na mafao yaliyolipwa na kwa mwaka 2010/2011 mifuko iliingiza Sh bilioni 575.63 ambayo ni asilimia 5.54 ya matumizi ya serikali ya Sh trioni 9.4,” alisema Mayingu.

Aidha, alizitaka taasisi za fedha na wataalamu wa uwekezaji kubuni njia na mipango ya kuwasaidia wastaafu ambao wanakiasi kikubwa cha fedha kitakachoweza kuchangia maendeleo.

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi alisema mkopo huo ambao ni wa kwanza katika soko la benki utawasaidia wastaafu kwani hauna dhamana.

Alisema mkopaji anaweza kukopa kuanzia Sh laki tano hadi milioni 20 kwa riba ndogo ya asilimia 12, zitakazolipwa kupitia pensheni yake ya mwezi ndani ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu.

Moshingi alisema tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo miezi sita iliyopita, zaidi ya wastaafu 2000 wameshanufaika na mikopo hiyo.

Akizungumza kabla ya kufungua huduma, Katibu Kiongozi mstaafu, Philemon Luhanjo alitaka kuwapo mafunzo maalumu kwa wanaokaribia kustaafu ili kuwajengea uwezo.

“Kuna haja ya kutoa mafunzo, na pia kuwapa ushauri wa namna bora ya kuwekeza na miradi ipi ya kufanya ambayo haina hasara kubwa na isiyo na shinikizo,” alisema.

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi