loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ramani bandia katika hifadhi za misitu ni kuihujumu nchi

Ramani bandia katika hifadhi za misitu ni kuihujumu nchi

Kwa siku nyingi inaelezwa kuwa baadhi ya watu wenye fedha, hutumia fedha hizo kwa maslahi yao binafsi. Katika kudhihirisha hilo, baadhi ya matajiri wanadaiwa kujimegea maeneo ya hifadhi mbalimbali, ikiwemo maeneo ya hifadhi ya mikoko jijini Dar es Salaam kwa kutumia ramani bandia.

Misitu mingine inayodaiwa kuvamiwa kwa mtindo huo ni Msitu wa Mikoko wa Delta ya Rufiji, Msitu wa Akiba na Nishati Morogoro/Mvomero na Msitu wa Kazimzumbwi (Chanika).

Habari hiyo ni moja ya tafiti, ambazo ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi, ambao wameporwa rasilimali hizo na watu hao wabinafsi, bila kujali uharibifu wa mazingira, unaosababishwa na uvamizi huo.

Utafiti wa hifadhi za misitu na mikoko nchini, uliofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya mazingira, umebaini ufisadi huo unaodaiwa kufanywa kwa kushirikiana na watumishi wa Serikali wasio waaminifu.

Ripoti ya utafiti huo inasema asilimia kubwa ya misitu nchini, iko hatarini kutoweka, ikiwa kasi ya uvamizi unaofanywa ndani ya hifadhi hizo hautadhibitiwa. Msaidizi Misitu Mkuu wa TFS Kanda ya Mashariki, Paul Ndahani alisema miaka 10 iliyopita, wananchi walivamia misitu na kuiba miti. Lakini, hivi leo wananchi wengi wenye fedha (matajiri) wamevamia misitu hiyo bila woga na kutengeneza mashamba na kisha kujenga nyumba.

Alitoa mfano wa Mkoa wa Morogoro, ambako wavamizi wa ardhi ya Hifadhi ya Msitu wa Akiba, wanatishia uhai wa hifadhi hiyo. Alisema matajiri wenye fedha, wamekuwa wakiingia ndani ya msitu na kujimilikisha zaidi ya ekari 300.

Anasema jitihada za kuwaondoa wavamizi hao, zinakumbwa na changamoto kubwa, ikiwemo vitisho, jambo ambalo linawawia vigumu kwa kuwa watu hao wanajulikana kwenye halmashauri na hata mkoani.

Mtafiti Charles Kayoka aliyefanya utafiti wa uharibifu wa maeneo ya Hifadhi ya Misitu kwenye maeneo hayo nchini, alisema hali ni mbaya na jitihada za haraka zinahitajika kunusuru mazingira.

Ukweli ni kuwa tuhuma hizo, zilizotolewa na wakala wa serikali ni kubwa na hatua za kisheria zinatakiwa kuchukuliwa haraka kushughulikia.

Alisema ikibainika kuwa tuhuma hizo ni za kweli, basi kitendo cha watendaji wa Serikali wasio waaminifu, kuchora ramani bandia na kuwauzia watu viwanja, kitakuwa ni uhujumu uchumi.

Nasema hivyo kutokana na ukweli kuwa ramani hizo bandia, licha ya kuwafanya watu wenye fedha kutumia maeneo hayo kinyume na utaratibu, pia husababisha uharibifu wa mazingira kwa matumizi mabaya ya hifadhi.

Ni vema wizara husika kuchukua hatua stahili kwa watendaji hao, wanaodaiwa kubadili ramani na matajiri wabinafsi ili kudhibiti hali hiyo isiendelee kutokea katika maeneo mengine ya hifadhi.

Nasema hivyo kutokana na ukweli kama tuhuma hizo, hazitashughulikiwa basi waliopewa majukumu ya kusimamia hilo, watakuwa wamesaliti wananchi kwa kushindwa kutimiza wajibu.

Ni vema serikali ichukue hatua stahili, ikiwemo kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyomegwa na matajiri, yanarudishwa serikalini na watendaji wote wasio waaminifu, wachukuliwe hatua kali kwa kitendo hicho.

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi