loader
RC aonya uchakachuaji takwimu za elimu

RC aonya uchakachuaji takwimu za elimu

Sekta ya elimu ili ifanikiwe inahitaji kuwepo na takwimu sahihi ambazo ni za uhakika zaidi ili kufanikisha utekelezaji wa mipango ya elimu.

Akifungua kongamano la siku moja la wataalamu wa elimu kutoka Halmashauri zote za Mkoa huo, Mongela alisema elimu ndiyo nguzo kuu na roho ya maendeleo katika taifa lolote duniani katika maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Aliwaambia wataalamu hao wa elimu kuwa mageuzi mbalimbali ya maendeleo, kiuchumi na teknolojia yanapatikana kutokana na maendeleo ya elimu.

Hata hivyo, Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha alisema udhaifu uliopo katika ukusanyaji wa takwimu za masuala ya elimu ni baadhi ya changamoto kubwa zinazoukabili mkoa huo na kikwazo kikubwa katika kuinua taaluma katika sekta ya elimu ngazi ya msingi na sekondari.

Mongela amewaambia viongozi hao wa elimu mkoani humo kuwa kudorora kwa elimu mkoani kunachangia na kukosekana kwa takwimu sahihi na za uhakika kutoka ngazi ya kijiji, kata na Halmashauri za Wilaya.

Aidha Mongela alisisitiza kwamba mafanikio katika uendeshaji wa elimu mkoani Arusha yatategemea kuwepo na usimamizi wa karibu wa uendeshaji wa sekta hiyo pamoja na wataalamu kuwajibika kikamilifu.

Mapema Ofisa Elimu wa Mkoa wa Arusha, Nestory Mloka alisema kongamano hilo linafanyika ili kujadili changamoto mbalimbali zinasababisha kushuka kwa kiwango cha taaluma katika shule za msingi na sekondari.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Prisca Libaga- Maelezo, Arusha

Post your comments