loader
Dstv Habarileo  Mobile
RC Dar awapa ‘kazi’ vijana wa ARS

RC Dar awapa ‘kazi’ vijana wa ARS

Sadiki amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuhakikisha timu zote za Ligi Kuu zinakuwa na timu za vijana.

“Kwa bahati nzuri, mashindano ya Airtel Rising Stars yamewapa fursa nzuri na ni vema timu za Ligi Kuu zikayatumia mashindano haya kupata vijana wenye vipaji na kuwaendeleza,” alisema.

Alisema mbali ya kuwa jukwaa la kubaini wachezaji wenye vipaji, Airtel Rising Stars pia yanawahamasisha vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwa na afya njema ili kukabiliana na masomo yao.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaambia vijana kwamba kwa dunia ya leo mpira ni chanzo cha kutumainiwa cha ajira kwa mamilioni ya vijana ambao wanaishi maisha mazuri kwa kuwa wanalipwa mishahara mizuri.

Aliwataka viongozi wa soka kuchagua wachezaji watakaoshiriki fainali za taifa kwa kuzingatia uwezo na siyo upendeleo wa aina yoyote. Wakati mashindano ya mkoa yakiendelea makocha watateua vijana wenye vipaji kuwakilisha mikoa yao kwenye fainali ya taifa na mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Gabon mwezi ujao.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa ameishukuru Kampuni ya Airtel kwa kubuni programu hii ili kutumika kama jukwaa linatotumika kubaini vipaji vya wanasoka chipukizi.

Alisema mashindano ya Airtel Rising Stars yameifanya kazi ya TFF ya kutafuta vipaji vya soka kuwa rahisi zaidi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando aliwashukuru wadau wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili.

Katika mechi ya ufunguzi iliyoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, timu ya Ilala iliiadhibu Buguruni Youth Center kwa 4-1. Mashindano hayo yanatarajiwa kuendelea leo kwenye Uwanja wa Karume.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi