loader
Redondo, Mwaipopo wasajili Villa Squad

Redondo, Mwaipopo wasajili Villa Squad

Usajili huo umefanywa chini ya ufadhili wa mdau wa soka, Nassoro Binslum ambaye tayari amesajili wachezaji 10 wazoefu kwenye kikosi hicho kilichodhamiria kutinga Ligi Kuu.

Villa Squad inajipanga kurudi Ligi Tanzania Bara msimu ujao, baada ya kushuka msimu wa 2011/12 pamoja na Polisi Dodoma na Moro United.

Kocha wa Villa Squad, Haji Issa alisema jana kuwa tajiri huyo ameunga mkono usajili huo ili kuongeza makali ndani ya kikosi chake baada ya kusajili wachezaji kutoka klabu kongwe ambazo zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Aliwataja baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Binslum kuwa ni Ramadhani Chombo ‘Redondo’ aliyeachwa na Simba, Ibrahim Mwaipopo kutoka Azam FC na Ally Mohamed ‘Gaucho’ aliyetokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Kocha huyo alisema wachezaji wengine ni siri kwa kuhofu kunyang’anywa na klabu ambazo hazijakamilisha usajili wao.

“Tunashukuru kuungwa mkono na Binslum ambaye anapenda maendeleo ya soka kiasi cha kutusaidia kuongeza idadi ya wachezaji wazoefu na tayari tumeanza maandalizi kuelekea kwenye michuano hiyo,” alisema Issa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Binslum kusaidia timu kutimiza malengo yake. Mbali na hiyo, anazifadhili Ndanda FC, Stand United na Mbeya City zinazoshiriki Ligu Kuu Tanzania Bara.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi