loader
RUBADA wahimizwa kutimiza malengo

RUBADA wahimizwa kutimiza malengo

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Christopher Chiza alitoa changamoto hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizindua bodi hiyo.

Alitaka wajumbe wake kufikia malengo waliyojiwekea na kuifanya Rubada kupiga hatua zaidi kimaendeleo.

“Ningependa kuona mnajiwekea malengo yenu na kutimiza kwa wakati ili mtakapomaliza muda wenu, mseme mliletea mafanikio mamlaka hii,” alisema Chiza.

Alisema wizara yake ina imani kubwa na bodi hiyo ambayo Mwenyekiti wake ni Profesa Lucian Msambichaka, ambaye ni miongoni mwa wachumi waliobobea nchini.

Mbali ya Profesa Msambichaka, wajumbe wengine katika bodi hiyo ni Profesa Henry Mahoo, Bashir Mrindoko, Gaspar Luanda, Hosea Mbise, Raphael Dalluti, Dk Ben Moshi, Eline Sikazwe na Nkuvililwa Simkanga.

Alitaka bodi hiyo kuharakisha upatakanaji wa sheria mpya ya mamlaka ili shughuli za uendelezaji Bonde la Rufiji zisikinzane na sheria nyingine.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Raphael Daluti.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi