loader
Ruvuma waagizwa kupanua wigo wa kodi

Ruvuma waagizwa kupanua wigo wa kodi

Agizo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga alipofungua mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT), uliofanyika mjini hapa.

Ngaga alisema viongozi wa Halmashauri, wasipokuwa wabunifu katika kuongeza mapato, hawatakwenda mbele na kuhudumia jamii, ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kama vile barabara na miradi ya kilimo.

“Tukijiongezea wigo wa mapato katika maeneo tunayowaongoza wananchi wetu, tutaweza kusonga mbele, ni vyema tuzingatie hilo”, alisema Ngaga.

Alisema Halmashauri ikitegemea chanzo kimoja cha mapato kufikia malengo iliyojiwekea, itakuwa ni vigumu na kusababisha kushindwa kutoa huduma husika kwa wananchi.

Pamoja na mambo mengine, Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza uboreshaji wa kiwango cha elimu katika shule za msingi na sekondari mkoani humo ili kuufanya mkoa huo, ufikie malengo mazuri ya ufaulu, ambayo imejiwekea katika sekta hiyo.

Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Misaada la taifa hilo ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Mbinga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi