loader
‘Sekta binafsi tangazeni vivutio vya Zanzibar’

‘Sekta binafsi tangazeni vivutio vya Zanzibar’

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Utangazaji, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk alipozungumza na wadau mbalimbali wa sekta hiyo ofisini kwake mjini hapa.

Alisema sekta ya utalii ni tegemeo kubwa katika kuingiza mapato ya nchi na fedha za kigeni, hivyo mchango wa kila jumuiya unahitajika kwa kiwango kikubwa.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mategemeo yake makubwa sasa ni katika mchango wa sekta ya utalii kuleta maendeleo,”alisema Mbarouk.

Aliwataka wawekezaji katika sekta hiyo na mawakala, kuhakikisha kwamba wanashiriki katika maonesho mbalimbali ya kimataifa duniani, kama njia ya kuitangaza Zanzibar na vivutio vyake.

Alisema Serikali tayari imeikabidhi sekta binafsi kuendeleza maendeleo ya utalii, hivyo mchango wao unahitajika kwa kiwango kikubwa.

“Wawekezaji katika sekta ya Utalii na mawakala miongoni mwa majukumu yenu ni kuitangaza sekta hii na kuona inapata mafanikio makubwa,” alisisitiza waziri huyo.

Baadhi ya mawakala katika sekta ya Utalii waliochangia katika kikao hicho, walisisitiza suala la ulinzi katika sekta ya utalii kuimarishwa.

Ofisa Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha na Kutembeza Watalii (ZATTI), Thabit Abdalla alisema wamesikitishwa na Jeshi la Polisi, kushindwa kutoa ushirikiano katika kupambana na wahalifu wakati matukio yanapotokea.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi