loader
Sekta binafsi yakaribisha uwekezaji kutoka China

Sekta binafsi yakaribisha uwekezaji kutoka China

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa kongamano la pili la biashara kati ya Tanzania na China juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye alisema taasisi hiyo inakaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo katika juhudi za kufikia maendeleo endelevu hapa nchini.

Kongamano hilo lilishirikisha kampuni zaidi ya 100 kutoka China na kampuni zaidi ya 120 za kitanzania.

Hadi sasa China imesajili miradi 522 kwenye Kituo cha Uwekezaji(TIC) yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 2.4 ambayo inatarajiwa kuzalisha ajira 77,335.

“Tunahitaji uwekezaji wao ufikie dola za kimarekani bilioni tano katika kipindi cha miaka mitatu ijayo,” alisema.

Alisema sekta binafsi inapenda waje kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda na siyo kutumia fursa waliyopewa na watanzania kuja kuuza bidhaa zao.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Raymond Mbilinyi alisema Tanzania imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha mazingira ya biashara ambayo yanavutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza kwa faifa ya nchi na wawekezaji.

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi