loader
‘Sekta ya makazi na upimaji haihitaji wachuuzi’

‘Sekta ya makazi na upimaji haihitaji wachuuzi’

Profesa Tibaijuka aliyasema hayo jana wakati akizindua banda la kampuni ya ujenzi la Property International Ltd, ambapo alisema amefurahishwa na teknolojia inayotumiwa na kampuni hiyo katika ujenzi wake ambao pia unasaidia kutunza mazingira.

Alisema asilimia 90 ya maeneo ya hapa nchini hayajapimwa hali ambayo inachangia kusababisha migogoro, kero na kesi za ardhi zisizokwisha.

Aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha katika eneo walilo nalo Kigamboni halikumbani na migogoro kati ya wakazi wa eneo hilo na viwanja vyao.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Abdulhaleem Salim alisema, kampuni yake ambayo ni ya wazawa ina lenga kuboresha maisha ya Watanzania hasa katika sekta ya makazi.

Alisema katika kipindi kifupi wameweza kupata ekari 200 ambazo zitakuwa na majengo ya kisasa. Alisema kati ya hizo mita za mraba 42,000 zimechukuliwa na Taasisi ya Kuwait kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya kisasa na mita nyingine kama hizo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Kisasa.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko na Katuma Masamba

Post your comments