loader
‘Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaendelea vizuri’

‘Serikali ya Umoja wa Kitaifa inaendelea vizuri’

Dk Shein alisema hayo wakati alipokutana na wenyeviti, watendaji na wajumbe wa bodi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema utendaji wa Serikali yenye muundo wa Umoja wa kitaifa ipo kwa mujibu wa ridhaa ya wananchi ambao wameiteua wenyewe.

“Nataka kuwaambia viongozi na wananchi kwa ujumla kwamba Serikali ya umoja wa kitaifa ipo kwa maslahi ya wananchi na viongozi waliopo madarakani tunaongoza kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Kwa mfano, Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekubalika mbele ya washirika wa maendeleo ambao wamekuwa wakitoa misaada yao bila ya matatizo.

“Serikali yetu ya Umoja wa Kitaifa imekubalika na washirika wa maendeleo ambao wamekuwa mstari wa mbele kutusaidia kwa sababu wametukubali,” alisema Shein.

Awali Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad alisema ushirikiano mzuri uliopo kati ya viongozi na watendaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa umesaidia kuleta utulivu na kujenga mazingira ya amani na utulivu.

Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa itapata mafanikio makubwa kama ushirikiano mkubwa utakuwepo kwa wananchi husika na wafanyakazi wa sekta mbalimbali ikiwemo serikalini.

“Ushirikiano mzuri ndio mafanikio ya ufanisi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo inaungwa mkono na wananchi,” alisema.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeundwa baada ya kuibuka kwa migogoro ya kisiasa na Zanzibar kuzuiwa kupewa misaada na mashirika ya kimataifa.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi