loader
Shein azindua ununuzi wa karafuu

Shein azindua ununuzi wa karafuu

Akizungumza na wakulima na wananchi, Dk Shein alisema karafuu ndio alama ya Zanzibar, hivyo ni wajibu wa wananchi kutunza na kuenzi zao hilo kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

Alisema serikali imefanya mabadiliko makubwa ya maendeleo ya zao hilo, ikiwemo kufanya mabadiliko katika Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).

Rais alipongeza shirika kutokana na kwenda sambamba na mabadiliko ya maendeleo, ikiwemo kujenga vituo vya kisasa vyenye hadhi ya zao hilo la karafuu.

Kwa mujibu wa rais, serikali imekuwa na mipango maalumu ya kuimarisha karafuu kwa kumpa mkulima asilimia 80 ya bei inayouzwa nje, kuzalisha miche 10,000 kila mwaka na kugawiwa wakulima bure na mpango wa kuilinda karafuu ya Zanzibar.

Alisema jitihada hizo za Serikali, zinapaswa kuungwa mkono na wakulima na wananchi kwa kuacha tabia ya kuchanganya karafuu na makonyo, kukaanga na kuanika barabarani.

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazurui alitangaza bei ya karafuu kwa mwaka 2014/2015 ni Sh 14,000 kwa daraja la kwanza, Sh 12,000 daraja na pili na Sh 10,000 kwa daraja la tatu.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi