loader
Shoprites waendelea kugoma

Shoprites waendelea kugoma

Miongoni mwa stahiki wanazozihitaji kutoka kwa mwajiri wao ni malipo ya likizo , matibabu, kiinua mgongo na mengine ambayo kwa muda mrefu walikuwa hawajapatiwa.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam , Msemaji wa Wafanyakazi hao Bahati Kalolo alisema hadi Aprili Mosi mwaka huu, kampuni hiyo itakuwa chini ya mwajiri mpya.

Alisema hofu yao si kupoteza kazi, bali ni kupoteza haki zao za msingi kama wafanyakazi.

Alisema kupitia Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) wamepeleka kesi Mahakama ya Kazi na Usuluhishi wakitaka kupatiwa stahiki zao.

Mgomo huo ulianza juzi kwa kuwakutanisha wafanyakazi wa maduka yote ya Shoprites ya jijini ambayo ni Mlimani City, Pugu na Kamata.

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi