loader
Shule yafungwa kwa watu kujisaidia madarasani

Shule yafungwa kwa watu kujisaidia madarasani

Kwa mujibu wa Mwenyikiti wa Kijiji cha Kibara B, Mafwili Mnyaga, shule hiyo imefungwa kuanzia Aprili 28, mwaka huu, baada ya kujitokeza hali hiyo.

Mafwili alisema kuwa shule hiyo iliyoko katika mji mdogo wa Kibara, wilayani hapa, imefungwa na wananchi wa kijiji hicho, baada ya walimu kukuta asubuhi kila chumba kimejaa kinyesi, milango, maeneo ya nje, pamoja na vyoo kutapakaa kinyesi.

Aidha, alisema kuwa mbali na hali hiyo pia mashimo ya vyoo hivyo vilikuwa vimezibwa kwa vitu vigumu, huku kinyesi kingine kikiwa kwenye ndoo za maji yanayotumiwa na wanafunzi kwa ajili ya kufanyia usafi.

Alisema kuwa baada ya walimu wa shule hiyo, ambayo iko katika katikati ya makazi ya watu, kukuta hali hiyo ambayo ilijitokeza siku hiyo asubuhi kwa kila darasa kuwa na kinyesi, ndipo walipotoa taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho.

Alisema kuwa baada ya kufika shuleni hapo na kufanya mkutano wa wananchi wote waliamua kuwatawanya wanafunzi na kisha kuifunga shule hiyo kwa muda usiofahamika.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kibara B, Tatu Bitenga, alisema kuwa walipoamka asubuhi ya siku hiyo walikuta hali mbaya sana, kwani kila sehemu kulikuwa na kinyesi kingi hasa kwenye madarasa yote manne ya shule hiyo, pamoja na vyooni.

Alisema kuwa tatizo kama hilo pia lilitokea Aprili 25, mwaka huu, ambapo walipoamka asubuhi walikuta hali kama hiyo na kutoa taarifa kwa Uongozi wa kijiji hicho.

Alisema mwanafunzi mmoja aliyeshiriki kufanya usafi katika chumba kimoja kilichokuwa na kinyesi aliugua ghafla ugonjwa wa ajabu na kuongeza kuwa hadi sasa hajahudhuria kwenye masomo.

“Mwanafunzi aliyefanya usafi kwenye chumba cha darasa aliugua ugonjwa wa ajabu na hadi leo hajahudhuria kwenye masomo,” alisema bila kuutaja ugonjwa huo.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Ahmed Makongo, Bunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi