loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yashusha nyota wawili

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliwataja wachezaji hao ni Jerome Ramatihakwana wa Botswana na Ousainou Menneh wa Gambia watakuwepo kwenye Tamasha la Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kaburu alisema Ramatihakwana na Kiongera watatua leo, wakati Menneh alitarajiwa kutua jana jioni.

Kati ya wachezaji hao, Kiongera tayari alifanya mazungumzo ya awali na kwa kushirikiana na wachezaji hao watapimwa afya na kuungana na wachezaji watakaokwenda katika kambi ya Zanzibar.

Wakiwa huko, Kocha Mkuu Zdravko Logarusic atawafanyia majaribio na baadaye atachagua mmoja atakayefuzu ili kusajiliwa msimu wa 2014/15.

“Baada ya Tamasha la Simba Jumamosi, kikosi kitaenda Zanzibar na wachezaji hao ambapo kutakuwa na mechi tatu za kirafiki kule. “Kocha ataangalia ni yupi anayemfaa ili kusajiliwa na kujumuisha kikosi cha mwisho kitakachoanza Ligi Kuu msimu ujao,” alisema Kaburu.

Kiongera bado ana mkataba wa miezi sita na timu yake ya KCB inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya.

Kwa upande wa Ramatihakwana, ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Botswana, lakini pia amewahi kucheza klabu za Mogoditshane Fighters, Mochudi Centre Chiefs, Santos na Vasco da Gama za Botswana, na mwaka jana alirudi kucheza Mochudi Centre Chiefs. Menneh anacheza Ligi ya Senegal.

Wiki hii, Simba ilifanya usajili wa mchezaji aliyekuwa akicheza Coastal Union ya Tanga, Abdi Banda kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka mitatu.

Tayari Simba SC imeshawasaini makipa Peter Manyika, Hussein Sharrif ‘Cassilas’, mabeki Jerome Mvengere, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Shaaban Kisiga na washambuliaji Ibrahim Ajibu, Elias Maguli na Mrundi Pierre Kwizera.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi