loader
SMZ kuendelea kujali walima karafuu kwa bei

SMZ kuendelea kujali walima karafuu kwa bei

Dk Shein aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na wakulima wa zao hilo wakati akizindua rasmi msimu wa ununuzi wa karafuu wa mwaka 2014/2015 uliofanyika katika ukumbi wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar –ZSTC huko wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.

Alifafanua kuwa kuwapatia wakulima bei hiyo ni miongoni mwa hatua nyingi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Saba kuhakikisha karafuu za Zanzibar zinaendelea kuwa na ubora wake na kubaki kuwa kitambulisho cha Zanzibar.

Dk Shein alizitaja hatua nyingine kuwa ni pamoja na kuimarisha huduma za ununuzi wa karafuu, kujenga barabara kwenye maeneo yenye karafuu nyingi, kutoa miche ya mikarafuu kwa wakulima, kutafuta masoko ya nje na kuwatia mikopo wakulima.

Hatua nyingine aliongeza kuwa ni kufanya uamuzi wa kulifanyia marekebisho makubwa shirika la ZSTC ili liweze kutekeleza majukumu yake kulingana na mazingira ya sasa na matokeo yake mafanikio makubwa yameonekana tangu mabadiliko hayo kufanyika.

Kabla ya uzinduzi huo, Rais alitembelea mashamba ya mikarafuu katika kijiji cha Tumbi –Chumbageni katika Wilaya ya Chakechake na kuona namna mkulima Said Sinani alivyoimarisha shamba lake la miaka mingi na shamba jipya la mikarafuu la wakulima Mbarouk Abdalla Mohamed na Songoro Shaaban Songoro.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Biashara, viwanda na Masoko, Ahmed Mazrui alitangaza rasmi bei ya ununuzi wa karafuu kwa msimu wa mwaka 2014/2015. Alitangaza bei hizo kuwa ni karafuu daraja la kwanza itakuwa ni 14,000/= kwa kilo, daraja la pili 12,000/= kwa kilo na daraja la tatu 10,000/= kwa kilo.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi