loader
Dstv Habarileo  Mobile
Takukuru waitwa Tanesco, TPDC Ewura, Madini

Takukuru waitwa Tanesco, TPDC Ewura, Madini

Ametaka Takukuru na vyombo vya dola kwa ujumla, kufanya uchunguzi kwenye Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) na Idara ya Madini.

Waziri Muhongo, alitoa agizo hilo kupitia hotuba yake kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo katika mkutano wake wa kwanza wa 2013/2014 wa siku mbili unaofanyika mkoani Morogoro.

Vitalu Kwa upande wa Idara ya Madini, Waziri alisema anawasiliana kiofisi na Takukuru ili watendaji wake wafike Makao Makuu wa Idara hiyo kuchunguza watendaji na wafanyakazi.

Sababu ya kuanza na Idara hiyo, Profesa Muhongo alisema ni kutoridhishwa na hatua ya viongozi kushindwa kufuta leseni za vitalu vya watu waliohodhi miaka mingi bila kuendelezwa kinyume na Sheria ya Madini.

Licha ya kusema sekta ya madini inakabiliwa na matatizo ya ucheleweshaji wa utoaji wa leseni na kushindwa kuwafutia wachimbaji ambao wamepewa vitalu vikubwa vya ardhi, imeonekana vinamilikiwa na wafanyakazi wake na vitatolewa kwa wachimbaji kwa njia ya rushwa.

“Inaonekana kusuasua kwa kushughulikia kutoa leseni kwa wachimbaji wanaohitaji na kuwafutia wale wanaoshindwa kuendeleza vitalu hivyo kunatia shaka, inaonekana vitalu hivyo ni vya baadhi ya wafanyakazi wa sekta ya madini ambao wametumia majina tofauti tofauti kuvimiliki.

“Kutokana na hali hii kwamba kuna uwezekano vitalu vingi vinashikiliwa na wafanyakazi wa Idara ya Madini, kuanzia Julai Mosi mwaka huu, Kamishna wa Madini asipovifuta kwa mujibu wa Sheria ya Madini nitaialika Takukuru waingie ili kufanya uchunguzi na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

“Tukiangalia tutagundua wafanyakazi wengi wa Idara ya Madini wamejichukulia vitalu vingi vya madini na kuwatafuta watu kwa kuwauzia kwa njia isiyo halali na jambo hili kimaadili na kisheria si sahihi. Takukuru itafanya kazi yake,” alisisitiza.

Aidha alitaka baraza hilo kupunguza mlolongo wa kupatikana kwa leseni za uchimbaji.

“Ni vyema kikao hiki cha Baraza kitoe majawabu kuhusu kuondoa urasimu huu, ili kuwezesha mwombaji apate leseni ndani ya siku mbili kutoka saba ama wiki mbili kutoka mwezi mmoja na kuwezesha wadau na wawekezaji kuvutiwa,” alisema Waziri Muhongo.

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi