loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanesco ishirikiane na jamii kutokomeza vishoka

Tanesco ishirikiane na jamii kutokomeza vishoka

Kisa cha kuomba hongo kwa watu hao ni madai waliyoyabuni ili kujipatia fedha kwa familia hiyo, wakidai mita ya Luku imechezewa, hivyo umeme uliokuwa ukitumika katika nyumba hiyo ni mdogo kuliko matumizi halisi ya nyumba hiyo.

Walitaka fedha hizo ili warudishe umeme, kwa madai kuwa zikilipwa ofisini, familia hiyo ingelipa adhabu ya Sh milioni nane, ambazo ni nyingi, ukilinganisha na zile wao walizotaka wapewe.

Familia hiyo ilifanya juhudi za kuwasiliana na Tanesco, ambao waliwatahadharisha kuwa watu hao ni mafundi vishoka na kuwataka watoe taarifa polisi.

Kisha familia iliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mmoja wa watu sita. Naipongeza sana familia hiyo na wengine ambao wamekuwa mstari wa mbele, kufichua maovu kama hayo, kwani wote tunajua ili kukomesha vitendo vya uhalifu ni lazima kila mtu awajibike kwa nafasi yake.

Tatizo la mafundi vishoka kutaka kuwaibia wateja wa Tanesco ni kubwa nchini na ni kubwa zaidi nje ya Dar es Salaam, ambapo wengi wao ni waoga au hawana uelewa na masuala ya umeme na teknolojia yake.

Kwani mbali na kujifanya wakaguzi wa mita za umeme, lakini pia watu kama hao huwadanganya wananchi kuwa watawaigizia umeme kwa haraka katika nyumba zao na kutaka wapewe kitu kidogo ili kupata huduma hiyo.

Kwa muda mrefu sana, kumekuwapo kwa madai na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoamini kuwa vishoka wa Tanesco, wamekuwa na ushirikiano wa karibu na baadhi ya watendaji wa shirika hilo.

Wananchi hao wamekuwa wakitupia lawama baadhi ya watendaji wa Tanesco kutokana na mafundi hao vishoka kuvaliwa sare na vitambulisho vya Tanesco, na hufika kwa wateja na kuwaeleza mifumo ambayo kwa hakika kama huna utaalamu, unaweza kuamini.

Kwa nyakati tofauti, watendaji wa Tanesco wamekuwa wakiwataka wananchi kuwa makini na vishoka na kukataa kuwalipa mafundi wa shirika hilo wakiwa nyumbani, badala yake wanamekuwa wakisisitiza malipo yafanyike katika ofisini.

Elimu inayotolewa na Tanesco, kuwasisitiza wananchi kuhakikisha malipo yafanyike ofisini, inaweza kusaidia kupunguza uhalifu. Lakini, kuna haja ya kwenda mbali kwa kushirikiana kwa karibu na watoa taarifa za uhalifu na polisi ili kutokomeza mtandao wao.

Pamoja na juhudi za familia hiyo kuijulisha Tanesco, inasikitisha kuwa watendaji wa shirika hilo, waliishia kutoa tahadhari kuwa watu hao huenda ni vishoka.

Majibu kama hayo kutoka Tanesco, hayakuwa dawa ya tatizo hilo, hasa ukizingatia kuwa shirika hilo ndilo linachafuliwa jina lake na watu wanahusisha kuwapo mtandao kati ya mafundi vishoka na watendaji wake.

Nilitarajia kuwa Tanesco wangekuwa mstari wa mbele, kuhakikisha watu hao wanakamatwa na kisha kwa kutumia polisi wataje mtandao wote wa watu wanaohusika kwenye wizi huo ili iwe rahisi kupambana nao, kama wako ndani ya shirika au nje.

Hivyo wakati umefika kwa uongozi wa Tanesco, kushirikiana na jamii hususani watu wanaotoa taarifa za uharibifu ili kuhakikisha wanatokomeza mtandao wa mafundi vishoka.

WIKI iliyopita umefanyika uzinduzi wa siku ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi