loader
Dstv Habarileo  Mobile
'Tanzania ina nafaka za kutosha'

'Tanzania ina nafaka za kutosha'

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea NFRA, kuona hali halisi ya hifadhi ya chakula na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari.

Alisema katika msimu wa mwaka 2014/15, NFRA inatarajia kununua tani 200,000, zikiwemo tani 190,000 za mahindi na 10,000 za mpunga.

"Msimu wa ununuzi unaanza hivi karibuni, na kwa kuwa NFRA ni moja ya wanunuzi wakubwa na wanaotegemewa na wakulima wengi na kwa kuwa akiba kubwa bado iko katika maeneo yanayozalisha mahindi kwa wingi, hatua zitachukuliwa kupunguza akiba iliyopo ili kupata nafasi kwa ajili ya hifadhi ya mavuno mapya," alisema.

Alisema kuwa Wakala unatarajia kuuza sehemu ya akiba yake ya tani 75,000 kwa soko la nje na ndani ya nchi ili kuacha nafasi kwa ajili ya ununuzi wa mazao mapya kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2014/15.

"Tani 50,000 zitauzwa nje ya nchi na tani 20,000 zitauzwa ndani ya nchi, wakati tani 5,000 ni kwa ajili ya taasisi za serikali," alisema Chiza na kuongeza kuwa mapato yatakayopatikana kutokana na mauzo hayo, yatatumika kuanzia ununuzi wa mazao mapya msimu wa 2014/15.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Charles Walwa alisema ili kupunguza malalamiko ya wakulima, kuhusu kutolipwa na baadhi ya mawakala wanaonunua mazao yao, NFRA imeweka utaratibu wa kuhakikisha wakulima hawanyonywi na mawakala hao.

Alitaja vigezo vinavyotakiwa na mawakala hao kuwa ni pamoja na kuwa na uzoefu wa kutosha, awe mtu aliyejisajili katika biashara ya kuuza mazao ya chakula, awe na leseni halali ya biashara, awe na hati ya usajili wa kodi na alipe ushuru wa mazao na kodi.

Vigezo vingine wakala anatakiwa kuwa na uwezo wa kuiuzia NFRA si chini ya tani kati ya 200 na 500 kwa mwaka, awe na mtaji wa kutekeleza angalau kwa asilimia 50 ya mkataba wake, awe na uwezo wa kuhifadhi angalau tani 50 za mazao ya nafaka na awe na utashi wa kumlipa mkulima kulingana na bei iliyowekwa na NFRA.

Hadi Juni 5 mwaka huu, Wakala ulikuwa umetoa tani 37,015.84 za chakula kwa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kukabiliana na upungufu wa chakula nchini.

Aidha, Wakala umeuza tani 24,490 kwa Shirika la Kimataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na tani 4,477 kwa ajili ya asasi zilizomo nchini. Hivi sasa Serikali ina jumla ya tani 176,061 katika maghala ya NFRA. Sehemu kubwa ya akiba hiyo iko katika maghala yaliyopo Songea, Rukwa, Mbeya na Iringa.

WACHEZAJI wa timu ya Shirika la ...

foto
Mwandishi: Ashery Mkama

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi