loader
Tanzania yaanza vyema kikapu Majeshi

Tanzania yaanza vyema kikapu Majeshi

Tanzania ambao ndio wenyeji, ilianza kwa kufungwa katika robo ya kwanza ambapo iliimaliza ikiwa na pointi 14-16 na kupoteza robo ya pili kwa kufungwa 18-15.

Kipindi cha pili, Tanzania ilionekana kuamka na kuanza kulenga mashambulizi langoni kwa wapinzani wao na kumaliza robo ya tatu wakiwa na pointi 24-13.

Miamba hiyo iliendelea kushambuliana kwa zamu huku kila timu ikionekana mashabiki wake kuimba na kupiga ngoma za asili za kwao, lakini mwishoni Tanzania iliibuka na pointi 67-56.

Mchezaji wa Tanzania, Mussa Maluga aliongoza kwa kuwa na pointi 19 akifuatiwa na Baraka Othman aliyekuwa na pointi 13, wakati Deo Nkurikinyika wa Rwanda akipambana na Fabrice Mugira wote wakiwa na pointi 12, wakifuatwa na Baptise Kabaiza aliyepata pointi 11.

Michuano hiyo ambayo inawashirikisha wanawake pekee, itaendelea leo kwa michezo miwili ambapo wa kwanza utachezwa asubuhi kati ya Uganda na Rwanda na jioni kutakuwa na mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Burundi.

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi